MHE. MCHENGERWA AMTEMBELEA PROF JAY MUHIMBILI

  Na. John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Mohamed Mchengerwa amemtembelea  aliyekuwa Mbunge wa Mikumi na Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Bw. Joseph Haule (Prof. Jay) anayetibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. 

 Mhe. Mchengerwa amefika leo Februari 12, 2022 kumjulia hali msanii huyo  na kuwasilisha salamu za Serikali kama msimamizi Mkuu wa Sekta ya Sanaa hapa nchini.

“Nimefika kumjulia hali mmoja wa wadau na miongoni mwa wasani ambao tunatambua na kuthamini  mchango wa kazi zake za sanaa ambazo zimehamasisha vijana wengi kujiajiri kupitia Sanaa ya muziki hapa nchini". Ameeleza Mhe. Mchengerwa

Tayari  Serikali kupitia Wizara ya Afya imesema itagharamia matibabu yake hadi hapo ataporuhusiwa kutoka hospitalini hapo.

Kwa upande wake mke wa Prof. Jay, Bi. Grace Mgonjo amemshukuru Mhe. Mchengerwa kwa upendo wa kuja kumwona msanii huyo .

Pia ameushukuru Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili  kuwapokea na kuwahudumia   vizuri.

Katika hatua nyingine Waziri Mchengerwa amewapongeza madaktari na wauguzi wa Hospitali hiyo kwa kazi nzuri wanayofanya ya utoaji wa matibabu ya kibingwa  kwa Watanzania.


Comments

Popular posts from this blog

Waziri Mchengerwa atoa wito kwa jeshi kuwa na timu ya soka.

Mhe. Kikwete aipongeza Wizara kwa kukuza Sekta ya Sanaa kwa kasi, adai ina mchango mkubwa kwenye uchumi

MOROCCO YAKUBALI KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KWENYE MICHEZO